Habari Njema Za

YESU KRISTO

Kwa Hatua 5 Rahisi

1

BINGU NI ZAWADI ILIYOTOLEWA BURE.
KAMWE HAIWEZI KUNUNULIWA WALA HAPANA ANAYESTAHILI.

*

Ni asubuhi ya siku ya kuzaliwa kwako. Mama yako amekupa zawadi ya bei ghali - simu ya rununu ya iPhone ya kisasa. "Ala! Shukrani Mama!" ukasema. Kisha ukatumbukiza mkono katika mfuko wako ili kutafuta fedha za kumlipa. Je, ukilipia zawadi ile, itakuwa ni zawadi? La! Haiwezi. Isitoshe, kujaribu kumlipa mama yako itakuwa kama kumtusi.

Ama kwa mfano, baba fulani ana nia ya kumhimiza mwanawe wa kike kwamba atie bidii masomoni, hivyo akamwambia, "Ukipata alama ya A katika kila somo mwaka huu, nitakununulia gari kama zawadi ya Krismasi."

Mwishoni mwa mwaka, binti yule kwa hakika apate alama za A, na kisha babake amnunulie gari. Je, ni zawadi? Hakika ni zawadi ya kupongeza bidii na matokeo yake bora.

Zawadi lazima itolewe bure na kwa hiari, na sharti ipokewe bure bila malipo. Iwapo utalipa ama kufanya kazi yoyote kama njia ya kulipa, basi sio zawadi.

Bibilia hutuambia wazi kuwa binguni (uzima wa milele) ni zawadi iliyotolewa bure.

Kwa maana Mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

Waefeso 2:8-9 NIV

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 6:23 NIV

Hakuna mtu awaye yote anayestahili nafasi binguni. Na hakuna mtu anayeweza kujipatia nafasi.

Sababu ni kwamba…

2

MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI.
HAWEZI KUJIOKOA.

*

Tutumie mfano huu; ulihitajika kuoka keki na kwamba kulihitajika mayai sita. Moja kwa moja, ukachukua yai na kulipasua kisha ukatia kiini chake katika bakuli. Ukachukua yai la mwisho na kufanya vivyo hivyo. Ghafla! ukageuza kichwa chako na kutazama upande mwinginene na kubana pua yako. Kumbe yai la mwisho lilikuwa bovu.

Ukawa huna la kufanya ila kuyamwaga yote. Ingawa mayai matano ni mazuri, yai moja bovu huharibu kila kitu.

Kama vile isivyowezekana kupakulia familia yako keki iliyookwa kwa yai bovu, hatuwezi pia kumpa Mungu mtakatifu, maisha yaliyoadhiriwa na dhambi, na kutarajia kuwa atayapokea.

Kiwango cha Mungu ki juu mno. Kwa upande wake, hasira ni sawa na mauaji; mawazo ya tamaa ya mwili ni sawa na usherati. Dhambi sio tu tufanyalo - bali ni kitu chochote tunachofikiri, kusema, kufanya au hata tusichofanya, kisicho kidhi kiwango kamili cha Mungu.

Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.

Warumi 3:23 NIV

"Lakini mimi ni muungwana," waweza kudhania. "Mimi hutunza familia yangu. Isitoshe, mimi hujitolea katika jamii yangu. Siibi wala kumuumiza yeyote. Hakika ni sharti niruhusiwe kuingia binguni?"

Iwapo unataka kuingia binguni kwa kujaribu kuishi maisha mazuri yenye haki, Yesu alisema hivi ndivyo inavyokupasa uwe:

Kwa hiyo iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Mathayo Mtakatifu 5:48 NIV

Kiwango cha kukufanya uweze kuingia binguni ni kuwa mkamilifu zaidi katika mawazo na matendo. Kwa ufupi, ni sharti uwe mkamilifu kama Mungu alivyo. Ni vigumu kwa binadamu kufikia kiwango hicho.

Pia, matendo mazuri hayawezi kutuokoa kwa sababu…

3

MUNGU NI MWENYE UPENDO NA HUTENDA HAKI.

*

Hebu tafakari haya; mtu aliyekata tamaa anaamua kuiba kwenye benki. Anatembea kuelekea kwenye karani wa fedha na kuelekeza mtutu wa bunduki, na kuamuru kwa hasira kwamba akakabidhiwe pesa.

Karani wa fedha aliyejawa na hofu anampa pesa.

Anachukua fedha zile na kuziweka kwenye fuko la takataka kisha anatembea haraka kuelekea mlangoni. Lakini ajapokuwa hajafika mlangoni, anateleza na kuanguka sakafuni kwa kishindo huku akiachilia bunduki. Walinzi wa benki wanamkamata.

Kotini, hakimu anamuuliza yule mwizi, "Je, unakubali au kukanusha mashtaka?"

"Naam, nakubali mashtaka." Hana lolote lingine la kufanya. Ushahidi uliotolewa dhidi yake ni thibitsho tosha.

"Mheshimiwa," mwizi anaendelea, "hili ni kosa langu la kwanza. Sikumjeuri yeyote. Benki ilirejeshewa pesa zote. Tafadhali, waweza kuyasahau haya yote na kuniweka huru?"

Je, hakimu atafanya haki iwapo atamweka huru mwizi yule? La. Sharti hakimu atekeleze wajibu wake na kufwata sheria. Sheria yasema wazi kuwa mwizi anafaa kuadhibiwa vikali.

Mungu ni mwenye haki zaidi kuliko hata hakimu. Kamwe hawezi kuruhusu au kutilia hamnazo uasi wetu.

...Mungu ni upendo.

1 Yohana 4:8 NIV

Lakini mimi [Mungu] siachi kumwadhibu aliyeasi.

Kutoka 34:7 NIV

Huu ndio utata: Mungu ni upendo wala hapendi kutuadhibu. Lakini pia Mungu hutenda haki na sharti aadhibu uasi wetu.

Mungu alitatua utata huu kwa kumtuma Yesu…

4

YESU NI MUNGU NA PIA MWANADAMU.
ALISULUBISHWA KWA AJILI YA DHAMBI ZETU.

*

Yesu ni Mungu aliye katika mwili wa binadamu. Si mtu muungwana, nabii au mwalimu tu.

Hapo mwanzo, alikuwako neno [Yesu] ; Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu….Neno akawa Mwandamu, na kwa neema na kweli, aliishi kati yetu. Tulishuhudia utukufu wake, utukufu alioupokea kama Mwana wa pekee wa Mungu.

Yohana 1:1 -14 NIV

Mungu anatupenda lakini ana chuki na dhambi zetu. Anatamani kuwa na uhusiano bora nasi. Lakini dhambi zetu ndizo ukuta unaotutenganisha naye.

Ili kutatua hili tatizo, Mungu alichukua dhambi zetu zote-za kale, za sasa na za wakati ujao- na kuzitua kwake Yesu. Kisha, akamwadhibu Yesu kwa ajili ya dhambi zetu.

Sote tulikuwa kama kondoo waliopotea, kila mmoja wetu akielekea kwenye njia yake. Lakini Bwana akachukua adhabu ile na kujitwika mwenyewe[Yesu], adhabu tuliyostahili sote.

Isaya 53:6 NIV

Yesu alikabidhiwa watu wakatili waliompiga na kumfedhehesha. Alipigwa usoni, akapigwa makofi, na kutemewa mate. Mwili wake ulinyofolewa na mijeledi iliyokuwa na ncha za vyuma.

Watu walipokuwa wakimcheka, taji la miiba likatiwa kichwani mwake. Kisha wakapigilia misumari miguuni na mikononi-alisulubishwa msalabani.

Mwishowe, alipokwisha kulipa hata deni la mwisho, Yesu alisema, "Tetelestai." Neno la kibiashara la hapo zama lililo na maana hiii: Deni limelipwa.

Yesu alikufa. Lakini siku tatu baadaye, Mungu alimfufua kutoka wafu.

Hii ina maana kuwa dhambi zako zimeshalipiwa ila tu si kwa mwili wako.

Yesu alikufa msalabani na kisha akafufuka kutoka wafu ili kulipia dhambi zetu na pia kununua mahali petu huko binguni. Mahali ambapo anatupa kama zawadi ya bure.

Kama ilivyo kwamba sabuni huwepo, lakini sabuni huondoa uchafu mwilini tunapoitumia - zawadi hio huwepo lakini hua ya maana pindi tunapoikubali.

Zawadi hii hupokewa kwa njia ya imani…

5

IMANI NDIO UFUNGUO
AMBAO HUFUNGUA MILANGO YA BINGU.

*

Kiokoa maisha cha mviringo kinaning'inia ukutani.

Ili kuweza kuingia kwenye akaunti yangu ya benki, inanipasa kuingiza nenosiri. Naweza kubahatisha nywila kadhaa. Lakini nenosiri sahihi pekee hufungua akaunti. Wokovu wenye imani ndio ufunguo wa kipekee wa kuingia binguni.

Je, nini maana ya kuwa na imani?

Mwanasayansi aweza kujua mengi zaidi kuyahusu maji, lakini iwapo yuko jangwani tena mwenye kiu, hekima aliyonayo haiwezi kumwokoa kutokana na kiu. Anahitajika kunywa maji. Kujua kwamba Mungu yupo sio wokovu wa imani.

Kabla ya kusafiri, tunaweza kumwomba Mungu atulinde, ama kabla ya kuanza mtihani twaweza kuomba kwamba Mungu atusaidie. Kumrudia Mungu wakati wa shida au jangaa pekee ni ishara tosha ya imani ya muda mfupi.

Wokovu wa Imani sio tu kutambua kuwa Mungu yupo, wala sio imani ya muda mchache. Wokovu wa imani wa kweli ni kumtumainia Yesu pekee kwa uzima wa milele.

Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?”
Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka-wewe pamoja na wa nyumbani mwako.”

Matendo ya Mitume 16:30-31 NIV

Hebu fikiri kwamba uko baharini kwenye meli. Umepatwa na dhoruba kubwa. Mawimbi yanayumbisha mashua yako ndogo. Hatimaye, meli yako ipate kuzama na ukawa kwenye barafu huku ukishikilia kipande cha mti.

Watu walioko kwenye meli nyingine wamekuona na wanakujia kwa haraka. Nahodha anapaza sauti, "Jamani! Nakurushia kiokoa maisha. Kichukue na ukishike. Tutakuvuta ili uwe salama."

Kwa njia hiyo hiyo, Mungu hutuona tukizama katika dhambi zetu. Hatuna nguvu za kujikwamua. Basi anatuita,"Nimekukabidhi kiokoa maisha. Jina lake ni Yesu. Achilia kipande cha mti. Mshikilie na nitakuvuta uwe salama."

Lazima tufanye uamuzi - kati ya kushikilia kipande cha mti (kujaribu kujiokoa wenyewe) ama kuachilia kipande hicho na kumwamini Yesu.

Yesu ndiye njia pekee ya uzimani. Ndiye mkombozi wa maisha yetu. Ili kuweza kupokea kipawa cha uzima wa milele ni sharti tumwamini Yesu.

JE, HAYA YANA MAANA KWAKO?

*

Ni wazi kuwa husomi haya kimakosa au kwa ajali. Mungu anakupenda. Angependa kukupa msamaha wa dhambi na pia mahali katika familia yake.

Je, ungependa kupokea uzima wa milele?

Hapana ibada wala mila ngumu utakayofuata. Zawadi hii hupokewa kwa kuomba.

Kama jibu lako ni ndio, tafadhali omba ombi hili:

Bwana Yesu. Mimi ni mwenye dhambi. Nataka kupokea kipawa cha uzima wa milele. Naamini kuwa u mwana wa Mungu. Naamini kuwa ulikufa kwa ajili ya dhambi zangu. Naamini kuwa ulifufuka. Nimeamua kukuamini. Asante Yesu kwa zawadi ya uzima wa milele. Amina.

Yesu alisema haya kuhusu ulivyofanya hivi punde:

Amin nawaambia, aaminiye anaye uzima wa milele.

Yohana 6:47 NIV

Hii ina maana kuwa tunapokea uzima wa milele pindi tunapoamini. Kwa sababu ya imani uliyo nayo, basi umepokea.

Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.

Yohana 1:12-13 NIV

U sehemu ya familia ya Mungu. Lolote ufanyalo haliwezi kubadili hilo - mtoto akisha zaliwa, hawezi kurudi tumboni.

Dhambi zako za hapo awali, za hivi sasa na zijazo zimesamehewa. Machoni pa Mungu, wewe ni, na daima utakuwa mkamilifu, kama vile Yesu.

WEWE SI MTUMWA WA HOFU TENA…

Mwana mikononi mwa babake.

Wewe Ni

MWANA WA MUNGU